Kituo cha Mafunzo kwa Mkulima (FTC), pamoja na kutoa mafunzo ni shamba la kilimo hai ambapo mbinu zote jumuishi za kilimo cha mazao ya msimu, uzalishaji wa nafaka kwa kutegemea mvua, ufugaji wa mifugo, kilimo misitu zinatekelezwa. Kituo hiki kipo eneo la Vianzi, kijiji kilicho umbali wa km 25 kutoka Morogoro mjini. FTC ni mahali pekee pakujifunza mbinu za kilimo hai. Aina mbalimbali za mafunzo hutolewa kwa wakulima binafsi, wakulima na wataalamu kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), mashirika ya kijamii (CBOs) na sekta ya umma.
Tulianzaje?
Kituo cha Mafunzo ya Mkulima (FTC) cha SAT kilifunguliwa rasmi Septemba 14, 2013, na kimeendesha kozi mbalimbali za mafunzo zilizohudhuriwa na wakulima na wataalamu kutoka Tanzania, Malawi, Kenya, na nchi za Ulaya. Tathmini na maoni kutoka kwa washiriki yamekuwa ya kutia moyo tangu hapo na yamekuwa daima kichocheo kwetu kuimarisha ubora wa kozi zetu.