KILIMO HAI HATUA YA PILI

Mafunzo ya kati ya kilimo endelevu

Wahitimu wa kozi ya "Misingi ya kilimo hai" kupatiwa maarifa zaidi kuhusu mbinu endelevu za kilimo hai. Sehemu ya kwanza ya kozi hii ni utangulizi wa kina zaidi kuhusu afya ya udongo na teknolojia ambazo zinaweza kutumika kuongeza rutuba ya udongo. Udhibiti wa visumbufu kwa kuzingatia mbinu za kilimo endelevu hufundishwa kwa vitendo na kinadharia. Pia, mbinu za kuhifadhi maji huwa ni lengo muhimu la kozi hii. Teknolojia mbalimbali za uzalishaji wa mazao pia huzingatiwa katika ufundishaji wa Kozi hii.


Utakayo Jifunza

Utajifunza yafuatayo;

  • Udongo, ‘kiumbe hai’ 
  • kuhuisha na kuboresha rutuba ya udongo
  • Viritubishi vya mimea
  • Utengenezaji wa Mboji na mbolea za majimaji

Malengo ya kozi

Malengo ya Kozi;

  • Washiriki kuongeza uzalishaji wa mazao yao kupitia utekelezaji wa mbinu walizojifunza.
  • Washiriki wanazalisha mbegu za mazao yao na hivyo kupunguza utegemezi kwa wasambazaji wa pembejeo za kilimo.
  • Washiriki kuhifadhi rutuba ya udongo katika mashamba yao kwa manufaa ya vizazi vijavyo

Kozi 2025

  • 13 Oktoba – 17 Oktoba 2025 — Course ID OAI 004

Tafadhali kumbuka kuwa ratiba yetu ya mafunzo inaweza kubadilika kwa sababu ya mahudhurio tofauti ya kozi. Ili kuthibitisha tarehe za kozi wasiliana nasi kama ilivyoonyeshwa hapa chini.

Ada ya Mafunzo: TZS 500,000 kwa kila mshiriki.

Fomu ya Usajili

Jisajili sasa kwa kozi zetu za mafunzo na upate ujuzi muhimu katika kilimo endelevu! Tafadhali jaza fomu hapo chini na taarifa zako za mawasiliano, chagua kozi unayotaka kuhudhuria na tarehe unayopendelea. Chaguo la malipo linapatikana wakati wa usajili.

-
+
Malipo ya Bank au Simu - (Kama simu, tafadhali andika namba)
KILIMO HAI HATUA YA PILI
14 Okt – 18 Okt 2024
Asante kwa kujisajili kwa kozi na sisi! Maelekezo zaidi yametumwa kwa anwani yako ya barua pepe. Tafadhali angalia kasha lako la kuingia (inbox) na kasha lako la barua taka (spam). Tunatarajia kukutana nawe katika kozi zetu za mafunzo. Ikiwa una maswali yoyote, tafadhali wasiliana nasi kupitia training@kilimo.org.
Oops! Something went wrong while submitting the form.