KAMBI YA VIJANA YA KILIMO

Je, kilimo ni biashara yenye faida kubwa ambayo vijana wanaweza kuwekeza?

Mafunzo haya ya wiki moja yanawafunza vijana katika mbinu za kilimo hai na stadi za Maisha ili kuonyesha jinsi gani kilimo kinavyoweza kuwa njia ya kujiajiri kwa vijana. Kozi hii imeundwa ili kuwafanya vijana kufurahia kukaa kwao katika Kituo cha Mafunzo ya mkulima kupitia michezo huku wakipata maarifa muhimu juu ya ukuzaji wa biashara ili kuboresha maisha yao.


Utakayo Jifunza

Utajifunza yafuatayo;

  • Uandaaji wa bustani na vitalu vya miti
  • Ujasiriamali na kilimo Biashara
  • Uchakataji wa vyakula na uongezaji wa thamani

Malengo ya kozi

Malengo ya Kozi;

  • Washiriki wanahamasishwa kujishughulisha na kilimo kama biashara kupitia uwezeshaji uliopo katika mazingira Rafiki kupitia mbinu shirikishi 
  • Washiriki wanaenda kuboresha Maisha yao kwa kuanzisha na kuendesha biashara za kilimo zenye faida
  • Washiriki wanauwezo wa kuunda fursa mbalimbali kupitia stadi za ujasiriamali waliojifunza kwa mfano utengenezaji wa sabuni, batiki, vitalu vya miti n.k

Kozi 2025

  • 11 Agosti – 15th Agosti 2025 — Course ID: AY 006
  • 8 Septemba - 12 Septemba 2025

Tafadhali kumbuka kuwa ratiba yetu ya mafunzo inaweza kubadilika kwa sababu ya mahudhurio tofauti ya kozi. Ili kuthibitisha tarehe za kozi, wasiliana nasi kama ilivyoonyeshwa hapa chini.

Ada ya Mafunzo: TZS 400,000 kwa kila mshiriki

(KUMBUKA: kila kitu kingine ni sawa na katika kozi ya kwanza)

Fomu ya Usajili

Jisajili sasa kwa kozi zetu za mafunzo na upate ujuzi muhimu katika kilimo endelevu! Tafadhali jaza fomu hapo chini na taarifa zako za mawasiliano, chagua kozi unayotaka kuhudhuria na tarehe unayopendelea. Chaguo la malipo linapatikana wakati wa usajili.

-
+
Malipo ya Bank au Simu - (Kama simu, tafadhali andika namba)
KAMBI YA VIJANA YA KILIMO
12 August - 16 August 2024
Asante kwa kujisajili kwa kozi na sisi! Maelekezo zaidi yametumwa kwa anwani yako ya barua pepe. Tafadhali angalia kasha lako la kuingia (inbox) na kasha lako la barua taka (spam). Tunatarajia kukutana nawe katika kozi zetu za mafunzo. Ikiwa una maswali yoyote, tafadhali wasiliana nasi kupitia training@kilimo.org.
Oops! Something went wrong while submitting the form.