Play Icon - Donate X Webflow Template
Watch video

Kituo cha Mafunzo kwa Mkulima (FTC) - Vianzi

Kituo cha Mafunzo kwa Mkulima (FTC), pamoja na kutoa mafunzo ni shamba la kilimo hai ambapo mbinu zote jumuishi za kilimo cha mazao ya msimu, uzalishaji wa nafaka kwa kutegemea mvua, ufugaji wa mifugo, kilimo misitu zinatekelezwa. Kituo hiki kipo eneo la Vianzi, kijiji kilicho umbali wa km 25 kutoka Morogoro mjini. FTC ni mahali pekee pakujifunza mbinu za kilimo hai. Aina mbalimbali za mafunzo hutolewa kwa wakulima binafsi, wakulima na wataalamu kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), mashirika ya kijamii (CBOs) na sekta ya umma.

Tulianzaje?

Kituo cha Mafunzo ya Mkulima (FTC) cha SAT kilifunguliwa rasmi Septemba 14, 2013, na kimeendesha kozi mbalimbali za mafunzo zilizohudhuriwa na wakulima na wataalamu kutoka Tanzania, Malawi, Kenya, na nchi za Ulaya. Tathmini na maoni kutoka kwa washiriki yamekuwa ya kutia moyo tangu hapo na yamekuwa daima kichocheo kwetu kuimarisha ubora wa kozi zetu.

KOZI ZINAZOTOLEWA KITUONI 

Kozi zetu

Usimamizi Endelevu wa Taka na mboji

7 Agosti - 11 Agosti 2023 — OAWM 005

Jisajili sasa kwenye Kozi ya Usimamizi Endelevu wa Taka na Komposti na ugundue jinsi ya kutumia taka kama rasilimali yenye thamani.

MAFUNZO KWA WAKUFUNZI WAWEZESHAJI

10th Jul – 14th Jul 2023
9th Oct – 13th Oct 2023

Je! unataka kuwa mwezeshaji imara katika kilimo?

Uhifadhi na usimamizi wa mazao baada ya kuvuna

4th Dec – 8th Dec 2023

Jifunze jinsi ya Kuhifadhi Mazao Baada ya Kuvuna na umuhimu wa kuhifadhi mazao yako

UCHAKATAJI WA VYAKULA NA UONGEZAJI THAMANI

6th Nov – 10th Nov 2023

Bidhaa zilizochakatwa na kuongezwa thamani huwa na bei nzuri, pia zinaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu, na zinachukua nafasi ndogo kwenye kuhifadhiwa.

KILIMO HIFADHI

18th Sep – 22nd Sep 2023

Endeleza shughuli zako za kilimo huku ukilinda mazingira ndio kusudi la mafunzo haya.

KILIMO CHA KUDUMU

21st Aug – 1st Sep 2023

Kilimo cha kudumu ni kozi inayotambulika kimataifa, inayoendeshwa kwa muda wa wiki mbili na utafanikiwa kupata Cheti cha kilimo cha Kudumu. Mafunzo haya yanatoa utangulizi wa kilimo cha kudumu ilivyofafanuliwa na mwanzilishi wake Bwana Bill Mollison.

UJASIRIAMALI NA KILIMO BIASHARA

4th Sep – 8th Sep 2023

Je, una nia ya kuanzisha biashara ya kilimo yenye mafanikio?

MADAWA YA ASILI KWA TINA ZA BINADAMU

4th Sep – 8th Sep 2023

Je! Unajua nguvu ya mimea?

KILIMO HAI HATUA YA PILI

23rd Oct – 27th Oct 2023

Mafunzo ya kati ya kilimo endelevu

Kilimo hai hatua ya tatu

27th Nov – 8th Dec 2023

Kilimo ikolojia hutumia rasilimali za asili ili kwa uzalishaji wa chakula bora na mifugo.

KAMBI YA VIJANA YA KILIMO

14th Aug – 18th Aug 2023

Je, kilimo ni biashara yenye faida kubwa ambayo vijana wanaweza kuwekeza?

UZALISHAJI WA MAZAO YA VIUNGO KWA MFUMO WA KILIMO HAI

18th Sep – 22nd Sep 2023
2nd Oct – 6th Oct 2023

Mahitaji ya mazao ya viungo ya kilimo hai yanazidi kuongezeka duniani kote na yanatarajiwa kuongezeka maradufu ndani ya miaka mitano ijayo.

Misingi ya kilimo hai

26th Jun – 30th Jul 2023
2nd Oct – 6th Oct 2023
20th Nov – 24th Nov 2023

Elewa misingi ya kilimo hai

MSINGI YA UZALISHAJI WANYAMA

17th Jul – 21st Jul 2023 (Introduction to poultry, piggery, and fish farming)
31st Jul – 4th Aug 2023 (Introduction to diary and beekeeping)

Je unafahamu, ufugaji na uzalishaji wa mazao unaweza kufanyika kwa Pamoja?